John 2:11-13

11 aHuu, ndio uliokuwa muujiza wa kwanza Isa aliofanya Kana ya Galilaya. Hivyo Isa alidhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

Isa Atakasa Hekalu

(Mathayo 21:12-13; Marko 11:15-17; Luka 19:45-46)

12Baada ya hayo, Isa pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, walishuka mpaka Kapernaumu, wakakaa huko siku chache.

13 bIlipokaribia wakati wa Pasaka ya Wayahudi, Isa alipanda kwenda Yerusalemu.
Copyright information for SwhKC